Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen ametangaza kwamba safari za ndege za moja kwa moja kati ya Nairobi na mji wa Brussels nchini Belgium.
Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Murkomen ameelezea kwamba safari hizo zitaanza Juni 3, 2024.
Kulingana naye, kampuni ya usafiri wa ndege ya Belgium itakuwa ikifanya safari sita kila wiki kati ya Kenya na Nairobi.
Aliyasema haya baada ya mkutano na balozi wa Belgium nchini Kenya Peter Maddens aliyekuwa ameandamana na meneja mkuu wa kampuni ya ndege ya Lufthansa katika eneo la Afrika mashariki Kevin Markette.
Hakikisho kutoka kwa wawakilishi hao wa Belgium Murkomen alisema ni dhihirisho la imani waliyonayo katika sekta ya uchukuzi wa angani nchini Kenya na mazingira ya biashara.
Hatua hii waziri alisema itatoa fursa za moja kwa moja na nyingine za ajira kwa wakenya wanaofanya kazi katika sekta ya usafiri wa angani jambo ambalo hatimaye litapiga jeki biashara na uwekezaji.
Watalii pia wanatarajiwa kuongezeka kutokana na safari hizo.