Rwanda ,Madagascar,Tunisia ,Zambia,Uganda na Afrika Kusini wameanza mashindano ya raga Afrika kwa wanawake kwa ushindi siku ya Jumamosi katika uwnaja wa RFUEA ,jijini Nairobi.
Madagascar wameshinda mechi mbili za kundi C wakiishinda Mauritius pointi 12-5, kabla ya kuwalemea Burkina Faso alama 36-12.
Uganda iliwabwaga Burkina Faso alama 45-0,nao Tunisia wakaicharaza Ghana 21-0, nao Zambia wakainyofoa Zimbabwe 36-5.

Mabingwa watetezi Afrika Kusini wameanza kutetea taji hiyo kwa ushindi wa 57-0.
Jumla ya mataifa 11 yanashiriki mashindano hayo yatakayokamilika Jumapili, huku mshindi akifuzu kwa mashindano ya msururu wa HSBC Sevens divisheni ya tatu mwaka ujao.