Rais William Ruto amesema serikali yake imejitolea kikamilifu kukabiliana na ufisadi.
Ruto amesema hayo siku ya Jumapili kwenye kikao cha mahojiano na wanahabari katika ikulu ya Nairobi.
Ameongeza kuwa maafisa wote waliohusika katika njama za ufisadi wa sukari, mafuta ya kupikia na pia mbolea ghushi tayari wamesimamishwa kazi na wanakabiliwa na mashtaka mahakamani.
Rais pia amewatea mawaziri husika katika wizara hizo akisema hawakupatikana na hatia ndio maana hakuwafuta kazi.