Rais William Ruto ameahidi kusitisha uagizaji wa samaki kutoka nchini China kama njia moja ya kuwainua wafugaji wa zamaki katika eneo la ziwa Victoria.
Akizungumza Ijumaa alasiri katika eneo bunge la Gem, alipohudhuria ibaada ya shukrani ya Mbunge Elisha Odhiambo,Ruto amesema hatua hiyo itawezesha ukuzaji wa samaki wengi katika ziwa Victoria na kuinua hali ya maisha ya wanaotegemea kilimo cha samaki.
Rais Ruto ameongeza kuwa serikali imewekeza shilingi laki tisa katika ziwa Victoria kujenga vituo vya kuopolea samaki .
Rais Ruto yuko kwenye ziara ya eneo la luo Nyanza anatazamiwa kuzuru kaunti zote nne za Kisumu,Migori,Homabay na Siaya kukagua na kufungua miradi ya maendeleo .