Ruto: Tumepiga hatua kubwa katika kufufua sekta ya sukari

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto amesema serikali yake imefikia hatua kubwa katika kufufua sekta ya sukari ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikisuasua. 

Ruto anasema ili kudhihirisha hilo, viwanda vyote 17 nchini kwa sasa vinafanya kazi huku viwanda vingine vinne vipya vikijengwa.

“Mwezi Julai pekee, uzalishaji wa sukari nchini ulifikia tani metriki 84,000 na kupita wastani wa matumizi ya taifa ya kila mwezi ya tani metriki 40,000,” amesema Rais Ruto katika hotuba yake kwa taifa leo Alhamisi.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya hivi karibuni, Kenya inazalisha sukari ya kutosha kukidhi mahitaji ya nchi.”

Kiongozi wa nchi amehusisha mafanikio hayo na mpango wa mbolea ya bei nafuu inayotolewa kwa wakulima wa miwa, ekari 500,000 za ardhi zinazotumiwa kwa upanzi wa miwa na usimamizi ulioboreshwa wa sekta hiyo.

“Nimetia saini tu sheria mpya ya sukari ili kutoa mwongozo zaidi wa sera huku tunapotafuta kuwa nchi inayouza sukari nje ya nchi,” aliongeza Rais.

 

Share This Article