Ruto: Tumebuni mazingira bora ya ukuaji wa uchumi

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto amesema nchi hii iko katika nafasi bora ya kukua kiuchumi kutokana na usimamizi bora wa uchumi wake. 
Amesema matumizi bora ya fedha na ulipaji madeni kwa njia mwafaka imeiondoa Kenya katika hatari ya kuelemewa na mzigo wa kushindwa kulipa madeni.
Amesema nchi hii iko thabiti kifedha na kutoa mazingira yanayohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi kuanzia Chini hadi Juu, BETA.
“Uchumi wetu uko katika njia ambayo itabuni nafasi zaidi za ajira na utajiri zaidi, uwekezaji wa fedha katika bidhaa za umma na huduma na kuipeleka nchi hii katika enzi ya ukuaji jumuishi,” alisema Rais Ruto.
Aliyasema hayo leo Jumatano wakati wa mkutano na wanahabari mjini Naivasha, kaunti ya Nakuru kulikofanyika mkutano wa pili wa serikali kuu.
Share This Article