Ruto: Sheria kufanyiwa marekebisho kuimarisha vita dhidi ya ufisadi

Martin Mwanje
1 Min Read
Serikali hivi karibuni itapendekeza mabadiliko kwa sheria husika ili kuziba mianya inayorudisha nyuma vita dhidi ya ufisadi nchini. 
Rais William Ruto amesema serikali kuu itafanya kazi pamoja na mfumo wa sheria kuhakikisha kesi za ufisadi zinamalizwa ndani ya miezi sita.
Amesema haitawezekana kamwe kwa mafisadi kukimbilia mahakama ili kukwepa kushtakiwa au kuchelewesha kupatikana kwa haki.
“Hatuwezi tukaendelea kuwavumilia wale wanaoibia umma kukimbilia mahakamani na kupata amri inayokataza wao kuchukuliwa hatua huku kesi zikiendelea kwa miaka kadhaa,” alisema Rais Ruto.
Aliyasema hayo leo Ijumaa wakati akikagua miradi ya maendeleo katika kaunti za Mombasa na Kilifi.
Ruto alisema marekebisho hayo ya sheria yanalenga kuimarisha uadilifu na kukabiliana vikali na ufisadi.
Alisisitiza dhamira ya serikali kutumia vizuri fedha za umma ili kuhakikisha Wakenya wanapata thamani ya fedha zao.
Aliyasema hayo wakati akiwa ameandamana na Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi na Magavana Abdullswamad Nassir (Mombasa), Gideon Mung’aro (Kilifi), Fatuma Achani (Kwale), Issa Timamy (Lamu) na Godhana Dhadho (Tana River) miongoni mwa viongozi wengine.
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *