Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama leo Jumanne jijini Accra, Ghana.
Ruto aliondoka nchini jana Jumatatu tayari kwa shughuli ya leo.
Rais mteule Mahama alimwalika Ruto kwa uapisho wake alipomtembelea nyumbani kwake Narok tarehe 29 mwezi uliopita.
Mahama aliye na umri wa miaka 66 alihudumu kwa muhula wa kwanza baina ya mwaka 2012 hadi 2017, akitwaa uongozi kufuatia kifo cha Rais John Atta Mills, kabla ya kushindwa na Nana Akuffo Addo mwaka 2017.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Mahama alipata asilimia 98 ya kura dhidi ya mpinzani wake Kojo Bonsu, aliyepata chini ya asilimia 2.
Ruto na mwenyeji wake Mahama wanatarajiwa kujadiliana maswala kadhaa ikiwemo ushirikiano katika sekta za nishati, nguo, diplomasia na biashara.