Ruto: Kenya, Somalia na Sudan Kusini kuboresha ushirikiano

Martin Mwanje
1 Min Read

Kenya imejitolea kuboresha ushirikiano na mataifa ya Somalia na Sudan Kusini kuhusiana na masuala ya maslahi ya pande mbili. 

Rais William Ruto amesema lengo la uboreshaji wa ushirikiano huo ni kupanua biashara kati ya mataifa hayo na kuhakikisha uthabiti na ustawi wa Afrika Mashariki.

Kiongozi wa nchi alisema ushirikiano huo hususan utasaidia katika kukabiliana na ugaidi, kutatua migogoro na kukuza amani ya kudumu Afrika Mashariki.

Ruto aliyasema hayo aliposhiriki mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Ali Mohamed Omar na mabalozi maalum wa Sudan Kusini Jenerali Akol Koor Kuc na Jenerali  Simon Makuac Yen katika Ikulu ya Nairobi.

 

Share This Article