Ruto: Kenya inakusudia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

Martin Mwanje
1 Min Read

Kenya imedhamiria kuongoza jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Hakikisho hilo limetolewa na Rais William Ruto wakati akiongoza taifa hilo kuadhimisha miaka 60 tangu lilipojinyakulia uhuru.

Rais Ruto amekuwa mstari wa mbele kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuungana kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambazo athari zake zinaendelea kushuhudiwa kila uchao.

“Najivunia kwamba tunaweza tukatekeleza jukumu muhimu katika kuongoza ajenda ya tabia nchi barani Afrika. Tumedhihirisha uongozi, ambao umetambuliwa ndani na nje ya bara la Afrika, na sharti tuendelee kutekeleza wajibu wetu humu nchini na katika jukwaa la kimataifa,” alisema Rais Ruto.

Alirejelea Mpango wa Viwanda Kijani barani Afrika uliozinduliwa kwa ushirikiano na Ufalme wa Milki za Kiarabu, UAE na viongozi mbalimbali wa mataifa ya Afrika wakati wa kongamano la tabia nchi, COP28 lililofanyika jijini Dubai.

Lengo la mpango huo ni kuziwezesha kampuni kujengwa kwa kasi humu nchini na barani Afrika kwa kutumia rasilimali za nishati mbadala.

 

Website |  + posts
Share This Article