Ruto awataka Mabolozi kunadi hatua za Kenya kuimarika kiuchumi

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais William Ruto amewataka mabalozi wanaohudumu humu nchini kuinadi Kenya vyema, hususan hatua zilizopigwa kiuchumi.

Rais amesisitiza kuwa uchumi thabiti ni kigezo muhimu kwa wawekezaji wa kimataifa humu nchini.

Aliyasema haya Jumamosi alipofungua kongamano la 19 la mabalozi jijini Nairobi.

Aidha, Ruto ametangaza kuwa Kenya itaandaa kongamano mbili za kimataifa zikiwa kongamano la Afrika na Ufaransa mwezi Mei na lile la bahari mwezi Juni

Share This Article