Rais William Ruto amesema ipo haja ya bara la Afrika kuwekewa masharti sawa ya mikopo na mataifa mengine ya ulimwenguni.
Ruto amesema haya Alhamisi alipozungumza katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa jijini Newyork.
Rais alisizitiza haja ya mataifa ya Afrika yanayozongwa na madeni kuondolewa mzigo ili yawe na uwezo wa kuzingatia maendeleo .
Kauli ya Ruto inafuatia taarifa ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyesema kuwa nchi 52 za Afrika zilizo na idadi ya jumla ya watu bilioni 3 nukta 4 yanakabiliwa na hatari ya kushindwa kulipa madeni.
Ruto aliongeza kuwa ipo haja ya mataifa yaliyo na mikopo kupewa mupumziko ya kutolipa madeni kwa kati ya miaka mitano hadi 10.
Ruto anahudhuria kongamano la 78 la umoja wa mataifa mjini Newyork.