Rais Ruto akutana na Obama

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku nne, alikutana na Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama katika makao yake ya Blair House.

Ruto alifanya mazungumzo na Obama kabla ya kulakiwa rasmi katika ikulu ya White House.

Obama ambaye alikuwa Rais wa 44 wa Marekani alizaliwa  na baba Mkenya na mama Mmarekani, na ailistaafu rasmi Januari 20 mwaka 2017 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Share This Article