Rais William Ruto amehudhuria uzinduzi wa kitabu cha Tawasifu ya Meja mstaafu Marsden Madoka katika Ikulu ya Nairobi.
Ruto ametamtaja Madoka kuwa aliyejituma kwa kazi yake na mchapa kazi shupavu aliyejitolea kulihudumia taifa.
Kitabu hicho kwa jina ‘At The Ready’ kinaangazia safari ya Madoka kutoka kwa familia maskini hadi utumishi wa umma na baadaye katika Ikulu.
Madoka aliye na umri wa miaka 82 aliteuliwa kuwa afisa wa polisi msaidizi wa Rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta ,alipokuwa na umri wa miaka 22 pekee.
Aidha Madoka alikuwa Mbunge wa Mwatate kati ya mwaka 1997 hadi 2007.