Rais William Ruto siku ya Jumamosi amehudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangu kubuniwa kwa jeshi la wanawamaji .
Hafla hiyo iliandaliwa katika makao makuu ya jeshi la wanamaji katika kivuko cha Mtongwe kaunti ya Mombasa .
Akizungumza kwenye hafla hiyo Ruto ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kupiga jeki na kuunga mkono jeshi la wanawamaji kupitia kwa ununuzi wa zana za kisasa na mitambo ya kiteknolojia, ili waimarishe ulinzi wa mipaka ya Kenya.
Rais pia amekariri kuhakikisha wanajeshi wanapokea mafunzo ya kisas,a ili kuongeza uwezo wake wa nguvukazi.
Aliwataka wanajeshi wa majini kutenda kazi kwa weledi na ustadi mkubwa.
Rais pia alizindua kitabu cha wanajeshi wa majini cha kuadhimisha miaka 60.
Jeshi la majini lilizinduliwa Disemba 12 mwaka 19964 mwaka moja baada ya Kenya kujipatia uhuru.