Ruth Chepng’etich ameweka rekodi mpya ya Dunia ya Marathon baada ya kushinda makala ya 46 ya Chicago Marathon nchini Marekani.
Chepng’etich amesajili rekodi mpya ya Dunia ya saa 2, dakika 9 na sekunde 56.
Amekuwa mwanariadha wa kwanza wa kike kukimbia marathon chini ya saa 2 na dakika 10, akivunja rekodi ya awali ya Tigist Assefa wa Ethiopia ya saa 2, dakika 11 na sekunde 53 ya mwaka 2022.
“Nahisi vyema, nafurahia matokeo yangu. Hii imekuwa ndoto yangu. Rekodi ya Dunia imerejea nyumbani na ni ushindi mahususi kwa marehemu Kelvin Kiptum, “alisema Chepng’etich aliyejawa na wingi wa furaha.