Riadha ya michezo ya Afrika kuanza rasmi Jumatatu nchini Ghana

Dismas Otuke
1 Min Read

Riadha katika mashindano ya bara Afrika nchini Ghana itaanza rasmi Jumatatu Machi 18, huku Kenya ikilenga kunyakua medali katika fainali za mita 3,000 kuruka viunzi na maji wanaume na mita 5,000 wanawake.

Fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji wanaume itang’oa nanga saa mbili tatu usiku bingwa wa zamani wa dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Amos Serem,Edmund Serem na Simon Kiprop wakiwajibika.

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji Beatrice Chepkoech atakuwa Mkenya pekee kwenye fainali ya mita 5,000 .

Mashindano ya riadha yakatakamilika Ijumaa hii.

Kenya ilinyakua medali 10 za riadha katika makala ya mwaka 2019 mjini Rabat,Morocco.

Share This Article