Rekodi ya Dunia ya Komen yavunjwa baada ya miaka 28

Dismas Otuke
1 Min Read

Rekodi ya Dunia ya mbio za mita 3,000 yake Mkenya Daniel Komen hatimaye ilivunjwa Jumapili jioni na Yakub Ingebrigsten wa Norway.

Ingebrigsten ambaye ni bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 5,000 alisajili rekodi mpya ya dunia ya dakika 7 sekunde 17.55, katika mashindano ya Silesia Diamond League nchini Poland.

Rekodi ya dunia katika mbio hizo za mizunguko saba unusu ya dakika 7 sekunde 20.67, ilikuwa imeandikishwa mwaka 1996 na Daniel Komen na ilikuwa imedumu miaka 28 kabla ya kuvunjwa.

Bingwa wa Dunia na Olimpiki Mondo Duplantis wa Sweeden pia alivunja rekodi yake ya Dunia ya kuruka kwa upote akisajili mita 2.26.

Share This Article