Reekado Banks atishia kufichua anayetatiza tasnia ya burudani Nigeria

Kulingana naye, huyo mtu huenda hajui analolifanya au anakatiza ndoto za wasanii wenye talanta makusudi.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Nigeria Ayoleyi Hanniel Solomon maarufu kama Reekado Banks, amesababisha minong’ono mitandaoni kufuatia ujumbe aliochapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa X.

Kulingana na mwanamuziki huyo, kuna tatizo kubwa katika tasnia ya muziki nchini Nigeria, huku akitishia kufichua mapepo yanayokabili tasnia hiyo.

“Siku moja nitakubali mahojiano kuzungumzia mtu aliye pembeni kwa tasnia ya burudani” aliandika mwanamuziki huyo.

Banks ambaye awali alikuwa amesajiliwa na kampuni ya kusimamia wanamuziki na kurekodi muziki ya Marvin Records inayomilikiwa na Don Jazzy, alizungumza kuhusu mtu fulani kwenye tasnia hiyo ambaye hajui anachokifanya au ni pepo tu.

“Huenda hajui anachokifanya au yeye ni pepo tu” aliendelea kusema Reekado akiongeza kwamba kwa njia moja au nyingine, watu walio na talanta za kipekee kuangukia mikono ya jamaa huyo.

“Labda kupitia hali ya kutojua lolote au kwa vitendo vya kipepo, watu hao wanakubali sera ambazo zinalemaza talanta zao au kusababisha waache kabisa kufuata ndoto zao maishani.” alisema Reekado.

Ujumbe huo wa Reekado ambao umevutia wengi umesababisha waanze kukisia anayemzungumzia huku wengi wakianzisha mazungumzo kuhusu changamoto ambazo wasanii wanakumbana nazo nchini Nigeria.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *