Real Madrid yamnyatia Mbappé

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Real Madrid imezidisha juhudi za kumnyemelea mshambulizi wa Paris St Germain Kylian Mbappé.

Madrid inawania kumsajili Mbappe kwa mara ya pili baada ya kumkosa katika dakika za mwisho za usajili wa mwezi Julai mwaka jana wakati Mfaransa huyo alipokubali kuongeza mwaka mmoja katika kandarasi yake na PSG.

Madrid tayari imewasajili Jude Bellingham, Joselu, Fran García na Brahim Díaz huku jezi nambari 9 iliyokuwa ikivaliwa na Karim Benzema aliyehamia Al Ittihida ikidokezwa huenda ikavaliwa na Mbappe.

Wakati huo huo, kiungo wa Croatia Luka Modric amesaini mkataba wa mwaka mmoja na vigogo hao wa Uhispania hadi mwezi Juni mwaka ujao.

Modric aliye na umri wa miaka 37, alitua Santiago Bernabeu mwaka 2012 na tayari ameshinda mataji 23 akiwa na timu hiyo katika kipindi cha miaka 11.

Website |  + posts
Share This Article