Klabu za Simba na Yanga zimekubali kurudi uwanjani kucheza derby ya Kariakoo ya Ligi Kuu Tanzania bara baada ya viongozi wa timu hizo mbili kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan, Ijumaa alasiri kwenye Ikulu.
Yanga walikuwa wameapa kutocheza na Simba kwa kile walihoji kuwa mapendeleo kutoka kwa wasimamizi wa Ligi hiyo.
Derby hiyo sasa itasakatwa Juni 25, katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkappa.
Yanga wanaongoza Ligi hiyo kwa alama 73,huku Simba ikiwa ya pili kwa alama 72, zikisalia mechi tatu msimu ukalimike.