APS Bomet kucheza Ligi Kuu FKF msimu ujao

PS wanashikilia nafasi ya pili Ligini NSL kwa ponti 64,alama 5, nyuma ya viongozi Nairobi United ikisalia mechi moja msimu ukamilike.

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Administration Police Service  Bomet  FC ,hatimaye itashiriki Ligi Kuu ya Kenya msimu ujao kwa mara ya kwanza baada ya kujihakikishia nafasi ya pili msimu huu kwenye ligi ya NSL.

APS wanashikilia nafasi ya pili Ligini NSL kwa ponti 64,alama 5, nyuma ya viongozi Nairobi United ikisalia mechi moja msimu ukamilike.

Timu hiyo ya Bomet ilipandishwa ngazi hadi Ligi Kuu msimu wa mwaka 2022,  baada ya kushinda Ligi ya NSL lakini msimju huo ukafutiliwa mbali baada ya FKF kuvunjiliwa mbali na serikali.

APS  watacheza mechi ya kufunga msimu kesho Jumamosi dhidi ya Mully Children’s FC .

Wakati uo huo Shirikisho la FKF limeipa APS alama 3 na ushindi wa mabao 2-0 kutokana na mchuano uliotibuka dhidi ya Kibera Black Stars Juni Mosi katika uwanja wa Jamhuri.

FKF imeipata Kibera Black Stars na hatia ya kuchangia kutibuka kwa mechi hiyo kunako dakika ya 79, wakati APS walikuwa wakiongoza bao moja kwa bila.

Website |  + posts
Share This Article