Raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yabainika

Dismas Otuke
1 Min Read

Droo ya mechi za raundi ya 16 bora kiwania taji ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya UEFA imetangazwa mkondo wa kwanza ukichezwa Februari mwakani na marudio mwezi Machi.

Katika Droo hiyo mabingwa watetezi Manchester City watakumbana na FC Copenhagen ya Denamark, wakati Arsenal ikipangwa dhidi ya FC Porto ya Ureno.

Mabingwa wa Ufaransa watamenyana na Real Sociadad,PSV ipimane nguvu na Borusia Dormund huku Lazio ikitoana jasho na Bayern Munich.

RB Leipzig itacheza dhidi ya Real Madrid,Napoli ichuane na Barcelona huku Intermilan ikimaliza udhia dhidi ya Atletico Madrid.

Mkondo wa kwanza wa raundi hiyo utacjezwa baina ya Februari 13 na marudio tarehe 5 mwezi Machi mwaka ujao wakati fainali ikisakatwa Juni mosi jijini London Uingereza.

Website |  + posts
Share This Article