Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza baraza jipya la mawaziri inayoshirikisha chama chake cha African National Congress, chama kikuu cha upinzani na vyama vingine tisa katika serikali ya muungano wa kitaifa.
Chama cha ANC kilipoteza umaarufu wake kwa mara ya kwanza baada ya miongo mitatu kwenye uchaguzi mkuu wa Mei 29 kikizoa asilimia 40 pekee .
Chama hicho tawala kilipata Mawaziri 20 kati ya mawaziri 32 huku chama cha Democratic Alliance, kikipata mawaziri sita huku nafasi nyingine sita zikigawanywa kati ya vyama vingine vilivyosalia .
Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance John Steenhuisen aliteuliwa waziri wa Kilimo.