Rais wa China Xi Jinping leo Alhamisi ametoa wito wa kusitishwa kwa vita katika eneo la Gaza na kuzuia kuzidishwa kwa mgogoro nchini Lebanon.
Xi ametoa wito huo wakati akihutubia viongozi wa nchi zinaobukia kiuchumi wakati wa mkutano wa BRICS.
“Tunahitaji kuendelea kushinikiza kusitishwa kwa vita katika eneo la Gaza, kuanzisha tena suluhu ya mataifa mawili na kusitisha kuenea kwa vita nchini Lebanon. Hakupaswi kuwa na mateso na madhara zaidi huko Palestina na nchini Lebanon,” Xi aliuambia mkutano huo nchini Urusi.