Rais wa Marekani Joe Biden, ameshikilia kuwa atawania Urais wa nchi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao, licha ya miito ya kumtaka ajiuzulu.
Hayo yanajiri huku ripoti ikitolewa kuwa Rais huyo mwenye umri wa miaka 81, ameambukizwa virusi vya COVID-19.
Mnamo siku ya Ijumaa wanachama wengi wa Democtrat walishinikiza kujiuzulu kwa Biden kutoka kwa kinyang’anyiro hicho, wakihofia huenda akashindwa na Donald Trump.
Kauli ya Biden ya kusema atawania urais, ilionekana kujibu wasiwasi wa baadhi ya wandani wake, kuhusu iwapo atasalia kwenye kinyang’anyiro hicho au la.
Maswali yameibuliwa kuhusu uwezo wa Biden kushinda Urais, hasaa baada ya kuonekana kusuasua wakati wa mjadala wa Urais dhidi ya mpinzani wake Donald trump mwezi uliopita.
Hata hivyo Biden alisema kuwa “Dau ni kubwa, na chaguo ni wazi. Kwa pamoja tutashinda,”.
Hadi kufikia sasa, wabunge 12 wa chama cha Democratic wanamtaka Biden ajiondoe katika kinyang’anyiro hicho, huku wakipendekeza Makamu wa Rais Kamala Harris kuchukua nafasi yake.