Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, ametoa amri ya kuuawa kwa kupigwa kwa mawe kwa wanandoa wa jinsia moja akisema ni kinyume cha imani zote za dini.
Rais Ndayishimiye ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kupinga mahusiano hayo amelaumu mataifa ya ulaya kwa kuchangia kueneza mienendo hiyo, na kuwataka raia wake walio katika mahusiano kama hayo kusalia ughabuni.
Kumekuwa na mjadala mkali kuhusu mahusiani hayo ya jinsia moja katika mataifa ya Afrika huku Rais wa nchini jiramni ya uganda ,Yoweri Museveni akipiga marufuku mahusiano hayo hali iliyochangia kufungiwa misaada na kuwekewa vikwazo na mataifa ya ulaya.
Uganda ndio nchi pekee ya Afrika mashariki iliyopitisha sheria ya kuharamisha mahusiano ya jinsia moja.