Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa katika kijijini Ngarash, wilayani Monduli leo siku ya Jumamosi.
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi,Rais mstaafui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jokaya Kikwete,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Philip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Hayati Edward Lowassa alifariki Februari 10,mwaka 2024 katika Hospitali ya Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipokea matibabu.