Rais Samia afanya uteuzi na utenguzi serikalini

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,amefanya uteuzi na utenguzi wa maafisa wakuu serikalini ili kuboresha utoaji huduma.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Ikulu ya Tanzania,Rais Samia amemteua  Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamadunu Sanaa na Michezo Said Othman Yakubu, kuwa balozi huku Mkurugenzi wa Habari Gerson Msigwa akitwaa nafasi ya Yakubu.

Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara Abdallah Mohammed amepigwa kalamu huku nafasi yake ikitwaliwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Elimu nchini Tanzania (TEA)Bi Bahati Ibrahim Geuzye ilihali nafasi yake katika TEA,ikajazwa na Erasmus Fabian Kipesha .

Mohammed Jumanne Gombati ameteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, huku Paul Kisesa akiteuliwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Bodi ya TANESCO.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini  Hanafi Msabaha amefurushwa nafasi yake ikikabidhiwa mkuu wa zamani wa wilaya ya Temeke, Bi Mwanahamisi Mkunda.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi Mariam Chaurembo amepigwa kalamu huku nafasi yake ikikabidhiwa Dkt Stephen Isaac Mwakajumilo.

Share This Article