Rais Ruto:Hazina ya michezo ikuze michezo pekee

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amemwagiza Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen kuhakiksiha hazina ya kustawisha michezo, inatumika kwa manufaa ya wanamichezo pekee.

Ruto amesema kuwa pesa hizo kamwe hazitatumika kutekeleza shughuli nyingine.

Rais amesema haya mapema Alhamisi katika Ikulu ya Eldoret, alipokutana na wanariadha wa Kenya walioshiriki michezo ya Olimpiki maajuzi jijini Paris.

Ruto amesema kuwa serikali yake inapanga kufungua akademia 25 za michezo  nchini, ili kukuza vipaji zaidi .

Share This Article