Rais Ruto yuko Tanzania kuhudhuria harusi ya bintiye Charlene

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais William Ruto na mkewe Rachel wako nchini Tanzania kuhudhuria harusi ya mwanao Charlene.

Charlene atafunga pingu za maisha na mfanyabiashara wa Tanzania Isaya Yunge.

Harusi hiyo itaandaliwa mjini Mwanza leo Ijumaa, Novemba 6 katika hoteli ya Malaika.

Rais Ruto anaandamana na wanawe na mbunge  wa Kapseret, Oscar Sudi miongoni mwa viongozi wengine.

 

Share This Article