Rais Ruto: Ukifikisha umri wa miaka 60, naomba ustaafu kwa amani

Martin Mwanje
1 Min Read

Watumishi wa umma wametakiwa kuhakikisha wanafunga virago na kwenda nyumbani punde wafikishapo umri wa miaka 60. 

Kumekuwa na visa vilivyokithiri vya watumishi hao kutaka kuongezewa muda wa kuhudumu hata baada ya kufikisha umri huo.

Hata hivyo, serikali inasema huku ikikabiliwa na changamoto za kifedha, kuanzia sasa hilo halitawezekana.

“Kuanzia sasa, watumishi wa umma wanaofikisha umri wa miaka 60 watatakiwa kustaafu mara moja bila muda wao wa kuhudumu kurefushwa,” alitangaza Rais Ruto wakati akihutubia taifa leo Ijumaa.

Hatua hiyo mongoni mwa hatua zingine lukuki zinazodhamiria kupunguza matumizi ya fedha za serikali na hivyo kuokoa fedha za kutosha zitakazotumiwa kufadhili miradi yenye manufaa kwa Wakenya.

Hatua zingine zinajumuisha kuwapiga maafisa wa serikali kushiriki hafla za michango almaarufu Harambee. Mwanasheria Mkuu ametakiwa kuandaa sheria itakayotoa mwongozo wa namna ya kuendesha hafla za michango nchini.

Imedaiwa kuwa wanasiasa hasa hupora mali ya umma ili kwenda kuitumia kwa kujinadi kwa wapiga kura na hivyo kuongeza uwezekano wao wa kuchaguliwa tena wakati wa uchaguzi.

Wakati huohuo, bajeti za siri katika afisi za maafisa wakuu serikalini ikiwemo afisi ya Rais sasa zitaondolewa, na bajeti za ukarabati serikalini kupunguzwa kwa asilimia 50.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *