Rais Ruto: Tuko tayari kutuma polisi Haiti

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametetea hatua ya serikali ya Kenya kutuma polisi nchini Haiti kulinda usalama.

Ruto amesema hatua hiyo ni mojawapo ya majukumu ya Kenya kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.

Ameongeza kuwa tayari Baraza la Mawaziri na Baraza la Kitaifa la Usalama limeidhinisha hatua hiyo na kulitaka bunge la taifa kutoa idhini jinsi inavyohitajika kikatiba.

Ruto alisema haya Jumamosi alipohudhuria siku ya kitaifa ya jeshi la Kenya katika kambi ya jeshi ya Embakasi.

Serikali ya Kenya inapanga kuwatuma maafisa wa polisi 1,000 kushika doria nchini Haiti.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article