Rais William Ruto siku ya Jumatano atazindua rasmi kanuni za ujenzi za mwaka 2024, pamoja na maabara za kuchunguza vifaa vya ujenzi Jijini Nairobi.
Kanuni hizo za ujenzi zilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali Februari 20, 2024, na zinalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya ujenzi na kufankisha ukuaji wa uchumi hapa nchini.
Aidha kanuni hizo pia zitawezesha mtazamo wa kisasa na maendeleo katika sekta ya ujenzi, kwa kuhakikisha usalama na uunganishwaji.
Mojawepo wa nguzo muhimu katika kanuni hizo ni kuhakikisha mijengo yote inawekwa kebo za mawasiliano kwa kuzingatia miongozo iliyopo ili kutosheleza mahitaji ya teknolojia.
Kanuni hizo za ujenzi zinazinduliwa huku serikali ya Rais Ruto, ikitekeleza ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kote nchini.
Kulingana na Rais Ruto, mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, umetoa nafasi za ajira kwa vijana huku nyumba hizo zikihakikisha wakenya wanapata nyumba bora za kuishi kwa gharama nafuu.