Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua programu mpya ya utoaji huduma zote za serikali maarufu kama GavaMkononi kuanzia majira ya saa nne asubuhi katika ukumbi wa KICC.
Programu hiyo itakuwa na huduma zaidi ya 5,000 kupitia kwa jukwaa la eCitizen huku ikirahisisha utoaji huduma na kuboresha ukusanyaji ushuru kwa serikali.
Baadhi ya huduma zinazopatikana katika programu ya GavaMkononi ni umiliki wa nyumba za gharama nafuu maarufu kama Boma Yangu.