Rais William Ruto anatarajiwa kuanza ziara ya siku nne katika eneo la Nyanza, ambapo atazindua na kukagua miradi kadhaa ya maendeleo.
Ziara hiyo itaanzia eneo bunge la Kuria Mashariki kaunti ya Migori Jumatano alasiri, kwa uzinduzi wa mradi wa maji wa Kegonga.
Rais pia atazindua mradi wa unyunyizaji maji wa Kuja katika eneo bunge la na barabara ya Ngere-Mapera katika eneo bunge la Suna Mashariki.n
Siku ya Alhamisi, kiongozi wa taifa atazindua mradi wa maji wa Oyugis katika kaunti ya Homabay.
Kisha ataelekea mjini Homa Bay kwa uzinduzi wa soko la kuuza samaki kabla ya kuelekea kisiwani Rusinga kwa uzinduzi wa barabara.
Rais Ruto pia anatarajiwa kuhudhuriwa ibada ya shukran ya Waziri wa Fedha John Mbadi katika eneo la Magunga, eneo bunge la Suba Kusini.
Siku ya Ijumaa kiongozi wa nchi atakuwa katika kaunti ya Siaya kuzindua mradi wa nguvu za umeme wa kisiwa cha Mageta kutokana na miale ya jua, na Kisha kuzindua siko la Siaya, kiwanda cha mchele na Kisha kuhudhuria ibada ya shukrani ya Waziri wa nishati Opiyi Wandayi.
Baadaye Rais Ruto ataelekea kaunti ya Kisumu siku ya Jumamosi kwa uzinduzi wa chuo cha mafunzo cha mabaharia na shughuli za baharini.
Rais atakamilisha ziara yake Kwa ukaguzi wa hospitali ya Lumumba.