Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa na baadhi ya viongozi wa eneo hilo, leo Ijumaa wamekaribisha ziara ya Rais William Ruto katika kaunti hiyo siku ya Jumamosi.
Katika ziara hiyo, kiongozi wa taifa anatarajiwa kuzindua mradi wa maji katika eneo bunge la Malava utakaoghatimu shilingi bilioni mbili na ambao utawanufaisha pakubwa wakazi wa Kakamega na maeneo karibu.
“Kaunti ya Kakamega inaunga mkono kikamilifu serikali jumuishi ya Rais William Ruto, na tunamkaribisha hapa Kakamega anapozindua mradi wa maji utakaogharimu shilingi bilioni mbili katika eneo bunge la Malava,” alisema Barasa.
Miongoni mwa viongozi walioandam,ana na Gavana Barasa ni pamoja na mbunge wa Malava Malulu Injendi na wawakilishi wadi David Ndakwa, Kevin Mahelo, Peter Wakukha, Peter Wanami, Geoffrey Sikolia and Keffa Musiya.