Rais William Ruto ameelezea kufurahishwa kwake na uhusiano mzuri wa muda mrefu uliopo kati ya Kenya na Msumbiji.
Amesema uhusiano huo umejikita kwa biashara na uwekezaji.
Kiongozi wa nchi amesema nchi hizo mbili zimeahidi kuboresha uhusiano huo ili kuongeza ujazo wa biashara ambao bado upo kiwango cha chini.
Ruto aliyasema hayo akiwa mjini Maputo nchini Msumbiji alikoanza ziara ya siku mbili leo Alhamisi.
Punde baada ya kuwasili, Ruto alifanya majadiliano na mwenyeji wake ambaye ni Rais Filipe Jacinto Nyusi mjini Maputo.
Aidha alishuhudia kutiwa saini kwa Makubaliano ya Maelewano saba katika nyanja mbalimbali za ushirikiano ikiwa ni pamoja usaidizi wa kisheria wa pande mbili, mafunzo ya kidiplomasia, mafunzo ya utumishi wa umma, uhamasishaji wa uwekezaji, uchumi wa Bahari na utambuzi wa pande mbili wa leseni za kuendesha magari.