Rais William Ruto amezindua ujenzi wa Soko la Kisasa la Eregi Shisejeri lenye thamani ya Sh89 milioni katika eneo bunge la Ikolomani, Kaunti ya Kakamega.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo.
Ruto pia ametangaza kuwa serikali imetenga Shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi wa masoko 24 ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Kakamega.
Aidha, Rais alizindua rasmi mradi wa kusambaza umeme almaarufu Last Mile Connectivity, ambao umetengewa Shilingi bilioni 2.5 a unalenga kuunganisha familia nyingine 36,000 na huduma ya umeme katika kaunti hiyo ya Kakamega.
Akizungumza na wakazi wa Shisejeri, Rais Ruto alisisitiza dhamira yake ya kuunganisha Wakenya bila kujali tofauti zao za kisiasa, akisema serikali jumuishi inalenga kuwaleta pamoja wananchi ili kutekeleza ajenda ya maendeleo yenye usawa.
Ruto yuko katika awamu yake ya pili ya ziara ya maendeleo katika eneo la Magharibi mwa Kenya, iliyoanza Novemba 28 na inayotarajiwa kukamilika Desemba 1, 2026. Ziara hiyo inahusisha kaunti za Busia, Bungoma, Kakamega na Vihiga.
Ziara hiyo inafuatia awamu ya kwanza ya ziara ya siku nne katika eneo hilo.