Rais William Ruto leo Jumatano amewateua watu wengine 10 kuwa mawaziri, juma moja baada ya kuteua nusu ya kwanza ya mawaziri.
Mawaziri walioteuliwa ni pamoja na:
- John Mbadi – Waziri wa Fedha
- Salim Mvurya – Waziri wa Biashara
- Rebecca Miano – Waziri wa Utalii
- Opiyo Wandayi – Waziri wa Nishati
- Kipchumba Murkomen – Waziri wa Masuala ya Vijana na Michezo
- Hassan Joho – Waziri wa Madini
- Dkt. Alfred Mutua – Waziri wa Leba
- Wycliffe Oparanya – Waziri wa Vyama vya Ushirika
- Justin Muturi – Waziri wa Utumishi wa Umma
- Stella Soi – Waziri wa Jinsia
Rais amesema atawasilisha majina hayo katika bunge la taifa ili yapigiwe msasa.
Alipokuwa akihutubia taifa Jumatano mchana katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto aliashiria kwamba angali anatekeleza mchakato wa kubuni Baraza jumuishi la mawaziri, na hivi karibuni atatangaza uteuzi zaidi.