Rais William Ruto amewasili Jijini Bürgenstock, Uswizi, kuhudhuria mkutano wa ngazi ya juu kuhusu juhudi za kuleta amani nchini Ukraine.
Kongamano hilo linalenga kubuni mikakati ya kwanza ya kuleta udhabiti katika taifa hilo la mashariki mwa bara Ulaya.
Washiriki wa mkutano huo wa Jumamosi na Jumapili, utajadili mapendekezo 10 yaliyotolewa na Ukraine ili kusitisha vita kati ya nchi hiyo na Urusi.
Rais Ruto anatarajiwa kuhutubia mkutano huo, huku akiangazia vita katika mashariki ya kati na Afrika.
Kiongozi huyo wa taifa pia atapigia kurunzi vita vilivyosahaulika barani humu, na athari zake katika ukuaji wa uchumi.
Zaidi ya viongozi 100 wa nchi na serikali wanahudhuria mkutano huwa wa siku mbili.