Rais Ruto awasili China kwa mkutano wa FOCAC

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto awasili nchini China kuhudhuria mkutano wa FOCAC.

Rais William Ruto na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga wako jijini Beijing, China kuhudhuria kongamano la ushirikiano baina ya China na bara Afrika.

Viongozi hao wawili ni sehemu ya ujumbe wa maafisa wa ngazi za juu wa kiafrika wanaohudhuria kongamano hilo.

Mkutano huo unatoa fursa kwa bara Afrika kuimarisha ushirikiano wake na China, kwa mujibu wa ujumbe wa rais Ruto kwenye ukurasa wake wa X, alipowasili Beijing.

Kwenye kongamano hilo Rais Ruto, ataangazia mikataba ya mabilioni ya dola na China, inayohusisha muundo msingi na biashara.

Wakati huo huo Raila atakutana na viongozi wa kiafrika kutafuta kuungwa mkono kwa azma yake ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika.

Wakati wa kongamano hilo linaloangazia kuimarisha na kujenga jamii ya ngazi za juu ya China na bara Afrika rais Ruto ataongoza kwa pamoja kikao kuhusu mpango wa biashara na muundo msingi.

Share This Article