Rais Ruto awarai Wakenya kushangilia WRC

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amewarai Wakenya kujitokeza kwa wingi kushangilia mashindano ya mbio za magari ya WRC Safari Rally.

Mashindano hayo yataandaliwa baina ya tarehe 28 na 31 mwezi huu mjini Naivasha.

Yatakuwa ya mkondo wa tatu baada ya mikondo ya Monte Carlo na Umea nchini Uswidi.

“Siku kuu hii ya Pasaka, najiunga na Wakenya kuwakaribisha madereva mashuhuri wa mashindano ya mbio za magari WRC Safari Rally mjini Naivasha,” alisema Rais Ruto.

Alitoa hakikisho la usalama kwa madereva wote wa kimataifa watakaoshiriki mashindano hayo.

“Nachukua fursa hii kuwahakikishia washiriki wote kuwa serikali itatoa usalama wa kutosha.”

Mashindano hayo yataanzishwa rasmi kesho Alhamisi katika ukumbi wa KICC na Rais Ruto, kabla ya madereva kuelekea Kasarani.

Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, madereva watashindana mjini Naivasha katika vituo vya Malewa, Loldia, Elementaita na Soysambu.

Share This Article