Ghana imemtunuku Rais William Ruto tuzo ya juu zaidi nchini humo inayojulikana kama “The Companion of the Order of the Star of the Volta.”
Akimkabidhi tuzo hiyo wakati wa dhifa ya kitaifa jana Jumatano jioni, Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alisema Rais Ruto ni “mfano wa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika” ambao wamesisitiza juu ya matumizi ya kanuni za uwajibikaji na kutii utawala wa sheria kwa raia wote bila kujali hadhi yao katika jamii”.
Aliongeza kuwa Rais Ruto amefanya hili bila kujali ugumu au hatari ya madhara ya kisiasa.”
“Chini ya uongozi wako, Kenya imekuwa mfano unaong’aa wa taifa linaloongozwa na utawala wa sheria,” alisema Rais Akufo-Addo.
Alisema chini ya uongozi wa Rais Ruto, Kenya imechukua tena nafasi yake ya majivuno katika jukwaa la kimataifa.
Alitaja mfumko wa bei unaopungua, ongezeko la kampuni zinazochipukia na idadi wa Wakenya wanaotarajiwa kunufaika kutokana na nyumba za bei nafuu na bima ya afya.