Rais Ruto atuma risala za heri njema za Eid Ul Fitr

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto ametuma risala ya heri njema kwa waisilamu nchini wakati huu wanaposherekea Eid Al Fitr.

Sherehe za Eid ul Fitr,  huadhimishwa baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Kwenye risala yake kupitia mtandao wa X, rais Ruto aliwatakia Waisilamu baraka za mwenyezi Mungu baada ya mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan.

Alisema mwezi wa Ramadhan ambapo waumini wa kiislam hufunga kula kwa saa kadha,ni ishara ya waisilamu kuzingatia maadili ya dini yao.

Alitoa wito kwa wakenya wote kusimama na Waisilamu wakati huu wa Eid ul Fitr na pia kuwakumbuka wale wasiobahatika katika jamii.

Rais Ruto alitoa wito kwa waisilamu kuendelea kuombea amani,umoja na ustawi wa taifa hili,  akiongeza kuwa ushirikiano baina ya wakenya wa dini tofauti ni msingi thabiti wa kudumisha amani,upendo na umoja nchini

Share This Article