Rais Ruto atia saini miswada minane kuwa sheria

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto atia saini Miswada minane kuwa sheria.

Rais William Ruto leo Jumatano,ametia saini kuwa sheria miswada minane ambayo ilipitishwa na Bunge la Taifa 

Miswada hio ni pamoja na ule wa marekebisho ya sheria ya Tume ya Ardhi wa mwaka 2023, mwada wa marekebisho ya Sheria ya Ardhi wa mwaka 2024, mswada wa uhifadhi wa na usimamizi wa Wanyama Pori wa mwaka 2023 na mswada wa marekebisho ya sheria ya matumizi mabaya ya tarakilishi na uhalifu wa kimtandao wa mwaka 2024.

Miswada mingine ni ule wa marekebisho ya sheria ya Tume ya Huduma za Polisi wa mwaka 2024, mswada wa marekebisho ya sheria ya ada za usafiri wa angani wa mwaka 2025, Mswada wa watoaji huduma za mali mtandaoni wa mwaka 2025 na mswada wa ubinafsishaji wa mwaka 2025.

Rais Ruto alisema sheria hizo zinatarajiwa kushughulikia dhuluma za kihistoria, kusimika usawa na uwazi na kupiga jeki ajenda ya ustawi na mageuzi katika taifa.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article