Rais William Ruto leo Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi, ametaja nusu ya kwanza ya Mawaziri 11.
Kiongozi wa taifa alisema atawataja mawaziri wengine hivi karibuni, hii ikiwa ni katika hatua ya kubuni serikali jumuishi.
“Nimeanza mchakato wa kubuni baraza jipya la mawaziri, litakalonisaidia kuleta mageuzi katika taifa letu,” alisema Rais Ruto.
Baada ya kuteuliwa, mawaziri hao sasa watasubiri kuidhinishwa na bunge kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.
Mawaziri hao ni pamoja na:
Prof. Kithure Kindiki – Waziri wa usalama na utawala wa taifa.
Dkt. Debra Mulongo Barasa – Waziri wa Afya.
Alice Wahome – Wizara ya Ardhi
Julius Ogamba – Wizara ya Elimu.
Aden Duale – Waziri wa Ulinzi.
Dkt. Andrew Karanja – Waziri wa Kilimo
Soipan Tuya – Waziri wa Mazingira.
Eric Muriithi – Waziri wa maji, usafi na unyunyiziaji.
Davis Chirchir – Waziri wa Uchukuzi na Barabara.
Dkt. Margaret Ndungu – Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi wa dijitali.
Rebecca Miano – Mwanasheria Mkuu.