Rais Ruto asifia kiwanda cha uvumbuzi cha Silicon Savannah

radiotaifa
1 Min Read
Rais William Ruto wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Silicon Savannah

Rais William Ruto amekilimbikizia sifa kiwanda cha uvumbuzi cha Silicon Savannah akisema kitatekeleza wajibu muhimu katika kuinadi Kenya kama kitovu cha teknolojia na uvumbuzi duniani. 

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi leo Jumatatu wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha Chuo Kikuu cha Nairobi, Rais Ruto amesema kiwanda hicho kinawiana na ajenda ya serikali ya kubuni nafasi za ajira za kidijitali.

Amesema uzinduzi wa kiwanda hicho hasa utasaidia kuimarisha juhudi za serikali za kukabiliana na ukosefu wa ajira na kuwapa vijana ujuzi wanaohitaji na kwa kufanya hivyo kuendeleza ukuaji wa uchumi jumuishi nchini.

Alitaja kiwanda hicho kuwa mfano bora wa ushirikiano wa kimataifa wenye maono.

Kiwanda hicho kinafadhiliwa na serikali ya Ufaransa kwa kima cha shilingi bilioni 4.7.

Share This Article