Serikali imesema itawiainisha mipango yake na ile ya serikali za kaunti, ili kuhakikisha ajenda ya maendeleo inaharakishwa hapa nchini.
Rais William Ruto, alisema hatua hiyo itashughulikia mahitaji ya wananchi na kuchochea ukuaji unaowajumuisha wote.
Kiongozi wa taifa aliyasema hayo Jumatatu katika Ikulu ya Nairobi, aliposhiriki mkutano na Magavana kutoka katikati mwa nchi, Mawaziri na Makatibu wa wizara.
Kupitia ukurasa wa X, kiongozi wa taifa alisema mkutano huo pia ulijadili kuhusu mipango na miradi muhimu inayotekelezwa kwa lenga la kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika eneo la mlima Kenya.
Baadhi ya wale waliohudhuria mkutano huo, ni pamoja na Naibu Rais Prof kithure Kindiki, Magavana Cecily Mbarire, Anne Waiguru, Kimani wa Matangi, Joshua Irungu, Muthomi Njuki, Irungu Kang’ata, Kiarie Badilisha na Isaac Mutuma.