Rais Ruto aongoza mkutano wa wabunge wa Kenya Kwanza

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumanne aliongoza mkutano wa wabunge wa muungano wa Kenya Kwanza katika Ikulu ya Nairobi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua na wabunge ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.

Wabunge wahudhuria mkutano wa wabunge wa Kenya Kwanza katika Ikulu ya Nairobi.

Mkutano huo unasadifiana na kuanza kwa  kikao cha Seneti kinachojadili kutimuliwa kwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza.

Vile vile, mkutano huo unajiri siku mbili tu kabla ya Rais William Ruto kuhutubia taifa  Novemba 9.

Share This Article